Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 37 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 479 2024-05-30

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Mlowo Wilayani Mbozi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2021/2022 hadi 2023/2024, Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 2.7 kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa maboma katika vituo vya kutolea huduma za afya katika Halmashauri ya Mbozi.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali itatenga shilingi milioni 600 kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mlowo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, ahsante.