Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 37 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 480 2024-05-30

Name

Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:-

Je, lini Serikali itamalizia ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Itenka – Nsimbo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali ilitoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Itenka ambapo majengo matano yamejengwa; jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD); jengo la maabara; jengo la upasuaji, jengo la wazazi; na jengo la kufulia. Aidha, jengo la OPD na maabara yamekamilika na yanatoa huduma tangu Mwezi Oktoba, 2022. Jengo la wazazi, jengo la upasuaji na jengo la kufulia yapo katika hatua ya ukamilishaji ambapo ili kuyakamilisha, kiasi cha shilingi milioni 100 kinahitajika. Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa awamu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa majengo hayo, ahsante.