Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 37 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 482 2024-05-30

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha kuweka changarawe katika barabara inayounganisha Tarafa za Umba, Mlalo, Mtae ya Hekicho, Lugurua hadi Manolo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, maeneo yanayotajwa na Mheshimiwa Mbunge yapo katika barabara ambayo imesajiliwa kwa jina la Kwekanda – Hekicho - Mkomazi yenye urefu wa kilomita 20.5 inayounganisha Tarafa za Umba, Mlalo, Mtae ya Hekicho, Lugurua hadi Manolo.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kujenga barabara tajwa kwa kiwango cha changarawe pamoja na kujenga miundombinu ya kupitisha maji ya mvua, ambapo mwaka 2021/2022 Serikali ilitumia shilingi milioni 500 kuifungua ili iweze kupitika.

Aidha, katika mwaka 2022/2023, shilingi milioni 201.5 zilitumika kujenga vivuko 14 vya maji, kuweka changarawe kilomita 8 na tabaka la zege mita 80 kwa baadhi ya vipande vyenye miinuko mikali. Ndani ya Mwaka 2023/2024 shilingi milioni 300 ilitumika kwenye uwekaji wa changarawe kilomita 7.2, tabaka la zege mita 110 na kujenga vivuko 5 vya maji.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa jumla ya kilomita 15.2 zimeshawekwa changarawe. Katika Mpango na Bajeti wa Mwaka 2024/2025, Serikali imetenga shilingi milioni 313 ili kukamilisha uwekaji wa changarawe, tabaka la zege mita 200, kujenga vivuko 7 vya maji ambapo barabara hiyo itaweza kupitika katika kipindi chote cha mwaka. (Makofi)