Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 4 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 51 | 2024-11-01 |
Name
Salim Alaudin Hasham
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ulanga
Primary Question
MHE. SALIM A. HASHAM aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Daraja linalounganisha Kata ya Mwaya na Mbuga lililovunjika tangu mwaka 2023?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha usanifu wa daraja la kudumu litakalounganisha Kata ya Mwaya na Mbuga ambapo inakadiriwa kugharimu shilingi bilioni 3.724 na kuwekwa kwenye mpango wa fedha za matengenezo ya dharura chini ya wabia ambao ni Benki ya Dunia. Kwa sasa, Serikali ipo kwenye hatua za mwisho kwenye mchakato wa manunuzi na utakapokamilika ujenzi wa daraja hilo utaanza mara moja.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved