Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 4 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 61 | 2024-11-01 |
Name
Issaay Zacharia Paulo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza Ujenzi wa Minara ya Simu katika Kata za Nahasey, Gunyoda, Silaloda na Marang - Mbulu Mjini?
Name
Jerry William Silaa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukonga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI K.n.y WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi, 2024, Serikali kupitia UCSAF, imetekeleza miradi katika Kata Tano za Wilaya ya Mbulu Mjini, ya ujenzi wa minara ya simu, ambapo miradi ya ujenzi katika Kata hizo imekamilika na wananchi wananufaika na huduma za mawasiliano. Aidha, katika Kata ya Nahasey, Kampuni ya Airtel ilikamilisha ujenzi wa mnara katika Kijiji cha Banee mwezi Machi, 2024.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali (Digital Tanzania Project) inaendelea na ujenzi wa minara katika Kata mbili za Gunyoda na Marang. Minara katika kata hizi inatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Mei, 2025 ambapo kukamilika kwa Kata hizi mbili kutaboresha huduma za mawasiliano ya simu katika Vijiji vya Banee, Hassama, Haysali, Nahasey, Gedamar, Gunyoda, Silaloda, Aicho na Gwandumehi na hivyo kuifanya Kata ya Silaloda kuwa na mawasiliano.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved