Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 4 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 63 | 2024-11-01 |
Name
Abeid Ighondo Ramadhani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Kaskazini
Primary Question
MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:-
Je, kuna mpango gani wa kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM aljibu:-
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 154 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura Na. 16 ya Sheria za Tanzania kinatamka bayana kuwa, vitendo vya mapenzi ya jinsia moja au mahusiano kinyume na maumbile, iwe faragha au kwa makubaliano ni kosa la jinai. Aidha, Kifungu cha 155 cha sheria hiyo, kinaweka adhabu kwa kosa la kujaribu kufanya vitendo vinavyokatazwa chini ya Kifungu cha 154. Hivyo, tutaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na Mahakama katika kusimamia utekelezaji wa Kifungu cha 154 na 55 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved