Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 4 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 64 | 2024-11-01 |
Name
Asha Abdullah Juma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza:-
Je, Serikali imejenga mabwawa makubwa mangapi nchini?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Serikali inaendelea na ujenzi wa mabwawa makubwa 18 ya umwagiliaji yenye jumla ya mita za ujazo milioni 321.89 katika Mikoa ya Dodoma, Tabora, Singida, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita, Mtwara, Lindi, Arusha, Tanga, Kigoma, na Manyara.
Mheshimiwa Spika, kati ya mabwawa hayo, ujenzi wa Bwawa la Tlawi Mkoani Manyara lenye mita za ujazo milioni 1.1, na ukarabati wa Bwawa la Ulyanyama, Tabora lenye mita za ujazo milioni 2.07 umekamilika. Aidha, ujenzi wa mabwawa 16 upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved