Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 8 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 130 2024-11-07

Name

Toufiq Salim Turky

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpendae

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kudhibiti ukuaji wa makazi katika maeneo ambayo hayajapimwa na kupangwa kuwa makazi ya wananchi?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa, katika kukabiliana na ukuaji wa makazi yasiyopangwa, imeendelea kuchukua hatua mbalilmbali ambazo ni pamoja na kuendelea kuandaa Mipango Kabambe (Masterplan) yenye dira ya kusimamia ukuaji wa miji. Aidha, Wizara imeanzisha miradi na programu mbalimbali kwa ajili ya kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi hapa nchini.