Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 8 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 133 2024-11-07

Name

Joseph Anania Tadayo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:-

Je, lini Serikali itafungua na kuanza kutumia Lango la Kaskazini la Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, lililojengwa Ndea, Mwanga?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Maliasili na Utalii ipo katika hatua mbalimbali za kufanya maboresho ya miundombinu ya utalii pamoja na kuongeza malango ya wageni ili kufanikisha watalii kufika katika vivutio vilivyopo kwenye Hifadhi za Taifa Tanzania, ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi. Kwa sasa ujenzi wa lango la kupokelea wageni katika eneo la Ndea, ndani ya Hifadhi ya Taifa Mkomazi umekamilika. Pia, barabara inayounganisha Hifadhi ya Taifa Mkomazi kupitia lango hilo na Wilaya ya Mwanga hadi kufika katika Kijiji cha Karamba, Ndea, yenye urefu wa kilometa 18 imeshafunguliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 78, kwa ajili ya kuiboresha barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe, ili iweze kutumika kwa shughuli za utalii katika msimu mzima wa mwaka. Ahsante.