Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 33 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 432 2024-05-24

Name

Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilosa

Primary Question

MHE. PROF. PALAMAGAMBA J. A. M. KABUDI aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Chanzuru hadi Melela – Kilosa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Chanzuru - Melela – Kilosa yenye urefu wa kilometa 64.5 imekamilika. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami, ahsante.