Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 33 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 433 2024-05-24

Name

Najma Murtaza Giga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza:-

Je, kwa nini Serikali isiweke kwenye mitaala somo la uraia na uzalendo ili kizazi kijacho kiwe na uelewa wa haki na wajibu wa raia nchini?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kutambua umuhimu wa kutoa elimu ya uraia na uzalendo kwa kizazi cha sasa na kijacho, ilifanya maboresho ya Mitaala ya Elimu mwaka 2023, ambapo katika maboresho hayo, tayari maudhui kuhusu elimu ya uraia na uzalendo yameingizwa katika mitaala hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kupitia somo jipya la Historia ya Tanzania na Maadili, litakalofundishwa kuanzia Elimu ya Awali hadi Kidato cha Sita, somo la Historia na Maadili litabeba maudhui yanayolenga kumjenga Mtanzania kuwa mzalendo na mwajibikaji anayefahamu historia, desturi, mila na maadili ya nchi yake, nakushukuru.