Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 33 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 434 2024-05-24

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO K.n.y. MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:-
Je, lini majengo ya Chuo cha VETA Chikundi – Ndanda yataanza kutumika?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa elimu ya mafunzo ya ufundi stadi katika kuimarisha ustawi wa uchumi wa wananchi katika Wilaya ya Masasi. Katika kutambua hilo, Serikali imejenga Chuo cha Ufundi Stadi katika eneo la Chikundi, Ndanda, Chuo ambacho kina jumla ya majengo 17 ambayo ni jengo la utawala, karakana nne, jengo la madarasa, majengo matatu ya maliwato, stoo ya vifaa, bwalo la chakula na jiko, jengo la mlinzi, jengo la kupokelea umeme, bweni la wavulana, bwei la wasichana, nyumba ya Mkuu wa Chuo na nyumba pacha kwa ajili ya watumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo hiki kwa sasa kimeshafunguliwa na majengo yote katika chuo hicho yanatumika. Aidha, katika mwaka 2023/2024 Chuo kimedahili wanafunzi na kuanza kutoa mafunzo, nakushukuru.