Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 34 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 448 2024-05-27

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuendeleza Kampeni ya kunawa mikono ili kudhibiti magonjwa ambukizi?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya uzinduzi wa Kampeni ya Mtu ni Afya kwa awamu ya pili ambapo inahimiza kuhusu kujengo vyoo bora, lishe bora, udhibiti wa taka, udhibiti wa magonjwa yasiyoambukiza sambamba na unawaji wa mikono kwa maji na sabuni.

Mheshimiwa Spika, kampeni hii imezinduliwa tarehe 9 Mei, 2024 na Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutekelezwa kwake kutawezesha kudhibiti magonjwa ambukizi katika jamii.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.