Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 34 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 451 2024-05-27

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. TUMAINI B. MAGESSA K.n.y. MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza: -

Je, lini ujenzi wa Barabara ya Kharumwa yenye urefu wa kilometa moja ya kiwango cha lami utakamilika?

Name

Innocent Lugha Bashungwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karagwe

Answer

WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hussein Nassor Amar, Mbunge wa Nyang’hwale, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Wingi 3 - Kharumwa – Nyang’holongo yenye urefu wa kilometa 68, sehemu ya Kharumwa yenye urefu wa kilometa moja umefikia 75% na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2024.