Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 49 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 637 2024-06-19

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza:-

Je, ni lini ujenzi wa Barabara ya Kiranjeranje – Nanjilinji – Ruangwa kwa kiwango cha lami utaanza?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Kiranjeranje – Nanjilinji – Namichiga – Ruangwa yenye urefu wa kilometa 120 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Kwa sasa maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Ruangwa Mjini hadi Namichiga (kilometa 20) yanaendelea chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia Mradi wa RISE ambapo mkataba wa ujenzi unategemewa kusainiwa mwezi Agosti, 2024. Kwa sehemu zilizobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha, kwa ajili ya kuendelea na ujenzi. Ahsante.