Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu 51 2025-01-31

Name

Tecla Mohamedi Ungele

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TECLA M. UNGELE aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka huduma za Mifuko ya Jamii ngazi ya Wilaya na Tarafa ili kuwaondolea usumbufu Wastaafu kwenda kuhakikiwa Mkoani?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tecla Mohamed Ungele, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa, kwa sasa uhakiki wa uanachama unafanyika katika Ofisi za Mifuko zilizopo mikoani na wilayani. Pili, Mifuko imefanya maboresho zaidi katika matumizi ya TEHAMA ambapo kwa sasa mstaafu anaweza kujihakiki mwenyewe kupitia simu janja (smartphone) kwa kutumia programu ya kidijitali (Online Portal) bila kuhitaji kufika katika Ofisi za Mifuko.

Mheshimiwa Spika, kwa maelezo hayo, ukusanyaji wa taarifa ni shirikishi toka ngazi zote zikiwemo ngazi za tarafa, wilaya hadi mkoani, ahsante.