Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 52 2025-01-31

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: -

Je, ni lini TARURA itaanza ujenzi wa barabara ya Vwawa- Iganduka hadi Isalalo kwa kiwango cha lami?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, barabara ya Vwawa - Iganduka hadi Isalalo ipo kwenye mpango wa uboreshaji wa miji na majiji chini ya Program ya TACTIC inayofadhiliwa na Benki ya Dunia katika kundi la tatu (Tier III), ambapo kwa awamu ya kwanza barabara yenye urefu wa kilomita 2.0 itajengwa kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, kuanzia Januari, 2025, wataalam wa usanifu wameanza kuripoti katika miji 18 ya kundi la tatu ikiwemo Halmashauri ya Mji wa Vwawa kuanza kazi ya usanifu kwa kipindi cha miezi sita. Baada ya usanifu kukamilika tunatarajia kutangaza zabuni za kuwapata Wakandarasi na washauri elekezi kupitia mfumo wa NeST ifikapo Juni, 2025 na taratibu za ununuzi zitakamilika Oktoba, 2025 ili Wakandarasi watakaopatikana waanze utekelezaji mara moja ndani ya mwezi huo wa Oktoba, 2025.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami katika Makao Makuu ya Miji ya Wilaya ikiwemo Vwawa, Songwe kulingana na upatikanaji wa fedha.