Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 8 2025-01-28

Name

Maida Hamad Abdallah

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA K.n.y. MHE. MAIDA HAMADI ABDALLAH aliuliza:-

Je, lini Serikali itawalipa madai ya muda mrefu Askari Polisi waliomaliza muda wao?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kulipa madai ya askari Polisi waliomaliza muda wao wa kazi baada ya kustaafu, jumla ya fedha kiasi cha shilingi 97,120,011,700.26 zinadaiwa. Mpaka sasa madai yaliyohakikiwa na kuwasilishwa Wizara ya Fedha kwa ajili ya malipo ni shilingi 75,214,744,005.10. Kwa sasa madai yanayoendelea kuhakikiwa ni ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 na kiasi cha fedha shilingi 21,905,267,695.16 zinadaiwa.

Mheshimiwa Spika, pindi uhakiki ukikamilika madai yote yatawasilishwa Wizara ya Fedha kwa ajili ya malipo. Ahsante.