Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Policy, Coordination and Parliamentary Affairs Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge 90 2025-02-04

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza: -

Je, Serikali inatumia utaratibu gani wa kuratibu na kutekeleza ahadi za Viongozi Wakuu nchini ili zisionekane ni za uongo?

Name

Ummy Hamisi Nderiananga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ina jukumu la kuratibu utekelezaji wa ahadi zinazotolewa na Viongozi Wakuu wa Kitaifa, wanaposhiriki katika matukio mbalimbali ya Kitaifa ikiwemo mikutano na wananchi pamoja na Kampeni za Uchaguzi Mkuu. Mara baada ya viongozi hao kutoa ahadi au maagizo, Ofisi Binafsi za viongozi hao kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu huziwasilisha kwenye Wizara za kisekta kwa ajili ya utekelezaji na kutoa mrejesho.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuhakikisha taarifa za utekelezaji wa ahadi hizo zinazowasilishwa zinakuwa na uhalisia, Ofisi ya Waziri Mkuu ilibuni na kuanza kutumia Mfumo wa Kielektroniki wa Uratibu na Ufuatiliaji wa Shughuli za Serikali (Dashboard). Mfumo huo, umeimarisha uratibu na ufuatiliaji wa ahadi hizo, kuweka kumbukumbu za ahadi hizo na kuwawezesha wataalamu kutumia muda mfupi kutuma maelekezo na kupokea taarifa za utekelezaji kutoka kwenye Wizara na Sekta husika, ahsante.