Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 6 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 94 | 2025-02-04 |
Name
Twaha Ally Mpembenwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibiti
Primary Question
MHE. TWAHA A. MPEMBENWE aliuliza: -
Je, ni nini mkakati wa Serikali kusaidia Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kupata Mapato kwa kuuza Carbon Credit?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa Biashara ya Kaboni kwa ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa kama ilivyoelezwa katika Kanuni ya Udhibiti na Usimamizi wa Biashara ya Kaboni nchini, Kifungu cha 15 - 18. Serikali inaendelea kubainisha fursa mbalimbali zinazopatikana katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo fursa ya kaboni katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti ambapo ikianza kuuzwa itaongeza mapato kwa halmashauri na wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa wadau watatu wameonyesha nia ya kuwekeza katika Biashara ya Kaboni kupitia rasilimali za misitu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti. Wadau hao ni pamoja na Amaly Asset Management LTD, TAZA Nature Company LTD na WWF.
Mheshimiwa Naibu Spika, halmashauri kwa kushirikiana na wadau walioonyesha nia ya kuwekeza kwenye kaboni wanaendelea kutambua maeneo yatakayoweza kutumika ili waweze kusajili miradi na kuanza uzalishaji kwa kuzingatia makubaliano ya Mkataba wa Paris Ibara ya Sita. Aidha, Serikali inazisisitiza halmashauri zote kote nchini zenye fursa ya misitu kuchukua hatua za kuanza biashara ya kaboni ili kuongeza mapato ya ndani na kuhifadhi misitu, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved