Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Works and Transport Wizara ya Uchukuzi 101 2025-02-04

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA aliuliza: -

Je, lini Wananchi wa Kiwanja cha Ndege Mwanza watalipwa fidia zao kwa kuwa tathmini imefanyika mara mbili sasa?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI K.n.y. WAZIRI WA UCHUKUZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Uchukuzi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Nyamagana zinaendelelea kukamilisha taratibu za uteuzi wa eneo ambalo litapangwa na kupimwa ili wananchi watakaoondolewa wamilikishwe kwa gharama nafuu. Katika zoezi hilo jumla Kaya zipatazo 1,404 zinatakiwa kupisha eneo la Uwanja wa Ndege wa Mwanza, ahsante.