Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo 105 2025-02-04

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuinua lugha ya Kiswahili kupitia vyombo vyake vya habari vya kitaifa?

Name

Hamis Mohamed Mwinjuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) inatekeleza mikakati mbalimbali ya kuinua na kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili kupitia vyombo vya habari vya kitaifa kama vile redio, televisheni, makala za magazeti na mitandao ya kijamii. Serikali imeweka msisitizo kwa vyombo vya habari vya kitaifa, kuandaa na kurusha vipindi vinavyoelimisha, kuburudisha na kuhamasisha matumizi ya Kiswahili fasaha.

Mheshimiwa Naibu Spika, vipindi hivi vinahusisha mijadala ya kitaaluma, tamthilia, mashairi, na makala zinazochambua masuala ya lugha na utamaduni. Kwa sasa idadi ya vipindi imeongezeka hadi kufikia 35 kwa wiki.