Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 6 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 107 | 2025-02-04 |
Name
Ally Anyigulile Jumbe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyela
Primary Question
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga Chuo Cha VETA Wilaya ya Kyela?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kujenga Vyuo vya Ufundi Stadi nchini ili kuwawezesha wananchi kupata ujuzi na mafunzo yatakayowawezesha wananchi kutekeleza kwa ufanisi shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kuzingatia fursa mbalimbali ambazo zipo kwenye maeneo yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ipo katika hatua za mwisho za makabidhiano ya Chuo cha Kyela Polytechnical College kilichokuwa kinamilikiwa na Kampuni ya KPC Limited.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeshaanza kufanya maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na kupeleka wanafunzi na vifaa kwa ajili ya mafunzo ili kuhakikisha kuwa chuo hiki kinaanza kutoa mafunzo mapema kikiwa chini ya Mamlaka ya VETA na kuwezesha Wilaya ya Kyela kuwa na Chuo cha Ufundi Stadi kama Wilaya nyingine zote nchini, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved