Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2000-2005 Session 12 Sitting 7 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 118 2025-02-05

Name

Rehema Juma Migilla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ulyankulu

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuruhusu maeneo ya hifadhi yaliyokosa sifa yatumike kwa matumizi ya kilimo na makazi?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia maelekezo ya Serikali imefuta mapori tengefu 12 yenye ukubwa wa ekari 707,962 kwa Tangazo la Serikali Na. 427/2020 yaliyokosa sifa na kurejeshwa kwa wananchi, kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, Wizara imefuta hifadhi za misitu saba zenye ukubwa wa ekari 46,715 kwa Tangazo la Serikali Na. 544/2020 zilizokosa sifa na kurejeshwa kwa wananchi, kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo makazi na kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hatua nyingine Wizara imetekeleza uamuzi wa Baraza la Mawaziri kwa kumega takriban ekari 973,380.906 kutoka katika maeneo ya hifadhi za Taifa, mapori ya akiba, mapori tengefu na hifadhi za misitu, kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya wananchi.