Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 127 2025-02-05

Name

Issaay Zacharia Paulo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga vituo vya Polisi Tarafa za Daudi na Nambis Wilayani Mbulu?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imetenga eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 2023 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi daraja C sehemu ya Chamulinga, Kata ya Daudi. Ujenzi wa kituo umepangwa kutekelezwa kwenye awamu ya pili ya mpango wa ujenzi wa vituo vya polisi vya kata unaoshirikisha Ofisi ya Rais, TAMISEMI katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Tarafa ya Nambis hakuna eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi vya kata. Ninaomba kutumia fursa hii kumshauri Mheshimiwa Mbunge pamoja na Halmashauri ya Mbulu kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Polisi vya Kata kwenye Tarafa ya Nambis. Ahsante.