Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 14 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 225 2025-02-14

Name

Masache Njelu Kasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupa

Primary Question

Hitaji la Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya - Chunya

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: -

Je, lini Serikali itatoa fedha za kujenga Ofisi mpya ya Mkuu wa Wilaya Chunya?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya lililopo lilijengwa mwaka 1937. Kwa sasa jengo hilo ni chakavu pamoja na juhudi za ukarabati unaofanywa mara kwa mara. Aidha, Serikali imeandaa michoro na gharama za ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya ambapo kiasi cha shilingi bilioni 3.5 kinahitajika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa kipindi cha maandalizi ya mpango na bajeti ya mwaka 2025/2026 kimefika, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya itawasilisha maombi hayo katika mpango na bajeti unaoendelea kwa ajili ya kupata fedha za ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya, ahsante.