Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 14 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 226 2025-02-14

Name

Zaytun Seif Swai

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Hitaji la Daraja Korongo la Oltukai – Monduli

MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga daraja katika korongo la Oltukai Kata ya Esilalei – Monduli?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2024/2025 Serikali imekamilisha usanifu kwa ajili ya ujenzi wa boksi kalavati ambapo gharama zilizobainishwa ni shilingi 170,000,000. Aidha, Serikali imetenga shilingi 600,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa daraja kwenye korongo la Oltukai pamoja na matengenezo ya barabara kipande korofi chenye urefu wa kilometa 2.5 ambapo barabara hiyo itachongwa na kuweka changarawe. Kwa sasa kazi hii ipo kwenye hatua za ununuzi.