Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 14 | Union Affairs | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 226 | 2025-02-14 |
Name
Asha Abdullah Juma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza: -
Je, Serikali imejipanga vipi kuongeza kasi ya upandaji miti ili kulinda mazingira?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuongeza kasi ya upandaji miti, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Wizara za Kisekta na Wakala wa Huduma za Misitu na wadau wengine imeendelea kuhamasisha ushiriki wa wananchi na sekta binafsi kupitia kampeni ya kitaifa ya upandaji miti millioni 1.5 kwa kila Halmashauri nchini ambapo kwa mwaka 2023/2024 jumla ya miti milioni 226.97 ilipandwa. Kati ya miti hiyo milioni 211.81 ilistawi sawa na 76%. Tathmini ya miti iliyopandwa kupitia kampeni hii kwa mwaka 2024/2025 inaendelea.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali imeendelea kutoa elimu kuhusu mazingira na kuhamasisha wananchi kupanda miti kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru ambapo kwa mwaka 2024/2025 jumla ya miti milioni 150 ilipandwa na Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar na miaka 60 ya Muungano ambapo kwa mwaka 2024 jumla ya miti 53,000 ilipandwa. Tathmini ya miti iliyopandwa kupitia utaratibu huu kwa mwaka 2024/2025 inaendelea.
Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia Bunge lako Tukufu, ninaomba kutoa wito kwa kila mwananchi na kaya kupanda miti ya aina mbalimbali ikiwemo miti ya matunda na kivuli ili kuweza kupata manufaa ya moja kwa moja yatokanayo na miti inayopandwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved