Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
1961-1995 Session 1 Sitting 1 Energy and Minerals Wizara ya Madini 227 2025-02-14

Name

Miraji Jumanne Mtaturu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mashariki

Primary Question

MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: -

Je, lini Serikali itawapatia leseni, mitambo na mitaji wachimbaji wadogo wa Jimbo la Singida Mashariki?

Name

Dr. Stephen Lemomo Kiruswa Mamasita

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Longido

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeweka utaratibu wa kuwapatia wachimbaji wadogo maeneo ya uchimbaji kwa kuwatengea maeneo maalumu na kwa kupitia mchimbaji mmoja mmoja kutuma maombi Tume ya Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, wachimbaji wadogo wa Jimbo la Singida Mashariki kama ilivyo kwa wachimbaji wengine wameendelea kupatiwa maeneo ya uchimbaji kupitia maombi ya mtu mmoja mmoja. Aidha, kwa upande wa maeneo yanayotengwa, Mkoa wa Singida umetengewa eneo la Mhintiri, Londoni na Sambaru kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata mitambo, Serikali kupitia STAMICO imesaini Hati za Makubaliano (MoU) na kampuni wazalishaji wa mitambo ya uchimbaji hapa nchini kwa lengo la kurahishisha upatikanaji wa zana na vifaa vya uchimbaji kwa wachimbaji wadogo. Kampuni hizo ni GF Trucks, Apollo Heavy Equipment’s na META. Katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata vifaa STAMICO pia kupitia vituo vya mfano inakodisha vifaa vya uchimbaji kwa bei nafuu. Vifaa hivyo ni pamoja na compressors na water pumps (pampu za kuvuta maji).

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu upatikanaji wa mitaji ya kuendeleza shughuli za uchimbaji mdogo, STAMICO imeingia makubaliano na taasisi za kifedha, zikiwemo benki za CRDB, NMB, Azania na KCB ili ziweze kuwakopesha fedha wachimbaji wadogo. Wizara kupitia STAMICO na Tume ya Madini imekuwa ikifanya semina na makongamano katika mikoa mbalimbali hapa nchini, kwa lengo la kuwafahamisha wachimbaji wadogo juu ya fursa zilizopo, ahsante sana.