Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 14 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 228 2025-02-14

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

Ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji – Itigi

MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga skimu nyingine ya umwagiliaji Itigi kwa kuwa iliyopo haifanyi kazi vizuri?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili kupata gharama halisi za ujenzi wa Bwawa jipya la Itagata pamoja na kuweka miundombinu ya umwagiliaji katika skimu hiyo.