Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 14 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 229 2025-02-14

Name

Tauhida Cassian Gallos Nyimbo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Mpango wa Serikali Kuwasaidia Wakulima Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS aliuliza: -

Je, Serikali imejipangaje kuwasaidia wakulima kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea na juhudi za kujenga uhimilivu wa athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta ya kilimo kupitia sera, mikakati na programu mbalimbali ikiwemo Ajenda ya 10/30, Mpango wa Mageuzi ya Kilimo pamoja na Mwongozo wa Kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi. Mikakati yote hii inalenga kuwasaidia wakulima kuongeza uhimilivu wa sekta kwa kutekeleza yafuatayo: -

(i) Uwekezaji katika kilimo cha umwagiliaji ambacho ni cha uhakika na himilivu ili kuepuka kilimo cha kutegemea mvua;

(ii) Ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora za mazao kupitia ASA ili kuhakikisha kwamba uhakika wa upatikanaji wa mbegu unakuwepo nchi nzima;

(iii) Utoaji wa mbolea na mbegu bora kwa mpango wa ruzuku;

(iv) Uwekezaji katika utafiti wa mbegu bora na zinazostahimili mabadiliko ya tabianchi kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI); na

(v) Uwekezaji katika mbinu na teknolojia himilivu ikiwemo kupima afya ya udongo, uboreshaji wa huduma za ugani, kuendeleza vituo mahiri vya kusambaza teknolojia na mafunzo ya kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi.