Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 14 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 230 2025-02-14

Name

Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Uhitaji wa Mbegu Bora za Minazi Mkoa wa Kilimanjaro

MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka mbegu bora za minazi katika Mkoa wa Kilimanjaro?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kuimarisha kilimo cha zao la nazi nchini ikiwemo kufufua kilimo cha zao hilo katika Mkoa wa Kilimanjaro kwa kuanza kuzalisha na kusambaza miche bora ya minazi asilia aina ya East African Tall kwa wakulima.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika msimu wa mwaka 2023/2024 Kituo cha TARI – Mikocheni kilisambaza miche 300 ya minazi aina ya East African Tall katika Mkoa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Same kwa ajili ya kupanda na kuanza kuzalisha zao la nazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha TARI Mikocheni kinaendelea kutoa mafunzo kwa wadau wote wa zao hilo ili kusaidia ufufuaji wa mashamba na kuongeza uzalishaji na tija kwa wakulima.