Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 14 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 231 2025-02-14

Name

Benaya Liuka Kapinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

Kuboresha Mfumo wa Malipo ya Kahawa – Mbinga

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kuboresha mfumo wa malipo ya kahawa ili kupunguza malalamiko ya wakulima kutolipwa malipo ya msimu?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuboresha taratibu za usimamizi wa masoko na mauzo ya kahawa zinazoweka mazingira wezeshi kwa wakulima na wafanyabiashara kufanya biashara kwa uwazi, kuongeza ushindani, kuimarisha bei ya mkulima na kupunguza malalamiko ya wakulima, hususani ucheleweshaji wa malipo ya kahawa waliyoiuza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kutatua changamoto ya kuchelewesha malipo, kuongeza ushindani na kuongeza ufanisi, Serikali kuanzia msimu ujao wa mwaka 2025/2026 itaendelea kuboresha mifumo ya masoko kwa kupunguza muda wa mkulima kusubiri malipo ya mauzo yake kutoka wiki mbili hadi saa 48 badala ya kahawa kuuzwa kwenye mnada.