Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 14 Water and Irrigation Wizara ya Maji 232 2025-02-14

Name

Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

Uhitaji wa Maji Safi na Salama Sambaru - Mang’onyi

MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza:-

Je, lini wananchi wa Kijiji cha Sambaru, Kata ya Mang’onyi Singida Mashariki watapata maji safi na salama?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Kijiji cha Sambaru kinapata huduma ya maji kupitia skimu ya maji ya muda mrefu ya Sambaru iliyojengwa mwaka 2003 wakati kijiji hicho kikiwa na watu 3,127. Aidha, kwa sasa kijiji hicho kina jumla ya watu 6,830 ambapo mahitaji yao ya maji yameongezeka kutoka wastani wa lita 78,175 kwa siku mwaka 2003 na kufikia lita 170,750 kwa siku mwaka 2025.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha kwamba kijiji hicho kinapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza Serikali katika mwaka huu wa fedha 2024/2025 itachimba kisima kirefu kwa ajili ya kupata chanzo cha uhakika cha maji kwa ajili ya kijiji hicho. Baada ya kisima kukamilika kazi ya usanifu wa miundombinu ya usambazaji maji pamoja na ujenzi wa mradi katika kijiji hicho utafanyika katika mwaka wa fedha 2025/2026.