Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 14 Water and Irrigation Wizara ya Maji 233 2025-02-14

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

Mradi wa Maji wa Ujuni Hadi Nkenja – Makete

MHE. FESTO R. SANGA aliuliza: -

Je, lini Mradi wa Maji wa Ujuni hadi Nkenja - Makete utaanza?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeshaanza utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Ujuni - Nkenja uliopo Wilaya ya Makete, Mkoani Njombe. Kazi zinazotekelezwa kupitia mradi huo ni pamoja na ujenzi wa chanzo (intake), ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 100,000, ulazaji wa mtandao wa mabomba umbali wa kilometa 26.4 pamoja na ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea maji. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025 na kunufaisha wananchi wapatao 6,432 waishio kwenye Vijiji vya Ujuni na Nkenja.