Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 14 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 234 2025-02-14

Name

Muharami Shabani Mkenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

Hitaji la Boti kwa Jeshi la Polisi – Bagamoyo

MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza: -

Je, lini Serikali itanunua boti na vifaa kwa Jeshi la Polisi Bagamoyo ili kudhibiti biashara za magendo na wahamiaji haramu?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia bajeti yake ya mwaka wa fedha 2023/2024 ilitenga fedha kiasi cha shilingi 4,500,000,000 ili kununua boti 11 kwa ajili ya matumizi ya Jeshi la Polisi katika kufanya doria maeneo ya baharini na ziwani. Boti sita zimeshawasili na zipo bandarini na taratibu za kutizoa zinaendelea. Pindi zikikamilika zitakabidhiwa Kikosi cha Polisi Wanamaji kwa ajili ya doria ya kudhibiti matukio ya uhalifu kwenye maji na maeneo ya Wilaya ya Bagamoyo yatafikiwa na kuhudumiwa, ahsante. (Makofi)