Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 14 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 235 2025-02-14

Name

Ndaisaba George Ruhoro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngara

Primary Question

Hitaji la Gari la Zimamoto – Ngara

MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itapeleka gari la zimamoto Wilayani Ngara hususani katika Mradi wa Rusumo?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Umeme wa Rusumo ulianzishwa kwa ushirikiano wa nchi tatu ambazo ni Tanzania, Rwanda na Burundi na unatekelezwa kupitia mikopo iliyotolewa na Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo Afrika. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeshiriki katika hatua zote ili kuhakikisha mradi huo unakuwa salama. Katika mradi huo, limenunuliwa gari moja la kuzima moto aina ya Mercedes Benz Acros 2036 (4x2) lenye ujazo wa lita 5000 za maji na lita 500 za foam. Aidha, gari hilo linatarajiwa kupokelewa na kukabidhiwa ifikapo mwezi Julai, 2025, ahsante.