Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 14 Defence and National Service Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa 238 2025-02-14

Name

Bakar Hamad Bakar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

Kuboresha Ofisi na Makazi ya Wanajeshi

MHE. ALI JUMA MOHAMED K.n.y. MHE. BAKAR HAMAD BAKAR aliuliza: -

Je, upi mpango wa Serikali kuboresha ofisi na makazi ya Jeshi la Wananchi nchini?

Name

Dr. Stergomena Lawrence Tax

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI K.n.y. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inatekeleza mpango mkakati wa miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2025/2026 wa kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuboresha mazingira ya kazi. Katika utekelezaji wa mpango huo, Wizara inaendelea na ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa – Kikombo, Dodoma, uboreshaji na ukarabati wa miundombinu mbalimbali katika vikosi, vyuo na shule. Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2025.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu makazi, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mpango wa nyumba 10,000 ambapo hadi sasa jumla ya nyumba 6,064 zimejengwa katika mikoa mbalimbali nchini. Vilevile Wizara inaendelea na ujenzi wa nyumba 3,936 zilizosalia kulingana na upatikanaji wa fedha za maendeleo. Aidha, Wizara inaendelea na ukarabati wa nyumba 6,064 katika maeneo mbalimbali ya Jeshi la Wananchi, ujenzi wa Hospitali Kuu ya Jeshi Msalato - Dodoma, uboreshaji wa Hospitali ya Kanda MH Mwanza na ujenzi wa mabweni ya maafisa na askari katika vikosi na viteule mbalimbali, ahsante sana.