Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 5 Policy, Coordination and Parliamentary Affairs Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge 70 2025-02-03

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Vituo vya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kila Mkoa

MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza:-

Je, Mikoa mingapi ina vituo vya kuwezesha wananchi kiuchumi, huduma zipi zinatolewa na wananchi wangapi wananufaika?

Name

Ummy Hamisi Nderiananga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia mwezi Januari 2025, jumla ya Vituo 27 vya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi vimeanzishwa katika mikoa 11 ya Shinyanga (vituo vitatu), Geita (vituo viwili), Kigoma (vituo nane), Katavi (kituo kimoja), Rukwa (kituo kimoja), Dar es Salaam (kituo kimoja), Tanga (kituo kimoja), Pwani (kituo kimoja), Morogoro (kituo kimoja), Dodoma (vituo saba) na Singida (kituo kimoja).

Mheshimiwa Naibu Spika, huduma zinazotolewa katika vituo hivyo, kwanza ni mafunzo ya ujasiriamali ambapo jumla ya wananchi 70,804 waliotembelea vituo hivyo wamepatiwa mafunzo hayo. Pili, kujenga uwezo kwa wafanyabiashara/wakulima ambapo jumla ya wananchi 18,708 walijengewa uwezo kupitia vituo hivyo. Tatu, kurasimisha biashara, ambapo jumla ya biashara 19,796 zimeweza kurasimishwa. Nne, kutoa ushauri wa kitaalamu ambapo jumla ya wananchi 8,806 wamepewa huduma za ushauri wa kitaalam. Tano, kutoa mikopo kwa wajasiriamali ambapo wajasiriamali 6,653 wamepatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 36.6. Ahsante.