Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 5 Community Development, Gender and Children Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu 71 2025-02-03

Name

Ng'wasi Damas Kamani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Uendelevu kwa Vijana Wanaonufaika na Program
za Ujuzi na Stadi za Kazi

MHE. NG'WASI D. KAMANI aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kutengeneza uendelevu kwa vijana wanaonufaika na programu mbalimbali za kukuza ujuzi na stadi za kazi?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Ng’wasi Damas Kamani, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mikakati ya Serikali katika kuhakikisha kuwa, kunakuwa na uendelevu kwa vijana wanaonufaika na programu mbalimbali za kukuza ujuzi na stadi za kazi ni ifuatavyo:-

(i) Kuwezesha vifaa/mtaji kwa vijana 1,621 walionufaika na mafunzo ya ufundi kupitia Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi;

(ii) Kushirikiana na Halmashauri zote nchini kupitia asilimia 10 ya fedha zinazotolewa au zinazokusanywa na Halmashauri kama pato ghafi, ili kuhakikisha wanufaika wote waliopata mafunzo ya ufundi kwa njia ya uanagenzi na urasimishaji wa ujuzi, nje ya mfumo rasmi, wanapewa kipaumbele kupata mikopo na zabuni zinazotangazwa katika Halmashauri hizo; na

(iii) Kuhakikisha mikopo inayotolewa na Mfuko wa Maendeleo wa Vijana unawawezesha vijana walionufaika na Programu ya kukuza ujuzi wanapata mikopo yenye masharti nafuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.