Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 12 | Enviroment | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 201 | 2025-02-12 |
Name
Anton Albert Mwantona
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Rungwe
Primary Question
MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha Taasisi zinazohudumia watu wengi zinaweka mifumo ya majiko ya gesi ili kuokoa mazingira?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha taasisi zinazohudumia watu wengi zinaweka mifumo ya majiko ya gesi ili kuokoa mazingira, Serikali imetekeleza jitihada mbalimbali za kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini. Baadhi ya jitihada hizo ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa Katazo la matumizi ya kuni na mkaa kwa taasisi za umma na binafsi zinazoandaa chakula na kulisha watu zaidi ya mia moja; ambapo jumla ya Taasisi 551 zimeanza matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa nishati safi ya kupikia; na kusaini makubaliano ya awali na wawekezaji mbalimbali wa makampuni ikiwemo Kampuni ya Oryx, Taifa Gas, Lake Gas na Manji’s gas kuhusu kutoa ruzuku ya shilingi Bilioni 8.64 kwenye nishati safi ya kupikia ili kupunguza mzigo wa gharama kwa watumiaji wa nishati safi ambapo jumla ya majiko 452,455 yamepata ruzuku. Aidha, Serikali inaendelea na ukamilishaji wa taratibu za kuanzisha Mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia ili kuweka ruzuku itakayowawezesha wananchi wa kipato cha chini kumudu bei ya gesi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha uandaaji wa Kanuni ya Katazo la Matumizi ya Kuni na Mkaa kwa Taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 kwa siku. Kanuni hizo zitajumuisha taasisi za umma na taasisi za watu binafsi. Ninakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved