Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 213 2025-02-12

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Primary Question

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza:-

Je, lini Wananchi wa Kata za Kasamwa na Nyamkumbu - Geita Mjini watalipwa fidia kutokana na alama za barabara kuwekwa katika maeneno yao?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wananchi wa Kata ya Kasamwa na Nyankumbu waliowekewa alama za X ya kijani ni wale ambao wamo katika eneo la hifadhi ya barabara lililoongezwa kutoka meta 22.5 hadi mita 30 kila upande kulingana na Sheria ya Barabara Na. 13 ya mwaka 2007 na Kanuni zake za mwaka 2009.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa uchambuzi wa kina unafanyika ili kubaini ni barabara zipi kweli zinahitaji upana wa eneo la hifadhi ya barabara wa mita 60 kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na hapo baadaye ya kuzipanua kulingana na ongezeko la wingi wa magari. Zoezi hili likikamilika taarifa ya Serikali itatolewa. Ahsante.