Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 2 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 26 | 2025-04-09 |
Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa barabara ya Nangurukuru – Liwale yenye urefu wa Km 231 utaanza?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Nangurukuru – Liwale yenye urefu wa kilometa 225.8 umekamilika. Ili kurahisisha kazi za ujenzi, barabara hii imegawanywa katika sehemu tatu, sehemu ya kwanza ni Nangurukuru – Zinga yenye urefu wa kilometa 78.7, sehemu ya pili ni Zinga – Choya (kilometa 71.4) na sehemu ya tatu ni Choya – Liwale (kilometa 75.7).
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya usanifu kukamilika, Serikali imeanza ujenzi wa sehemu ya tatu ya Liwale – Choya (kilometa 75.7) ambapo zabuni kwa ajili ya ujenzi wa kipande cha kilometa 10 kutoka Liwale kuelekea Choya zimetangazwa tarehe 3 Februari, 2025 na kwa sasa iko katika hatua ya uchambuzi (evaluation). Kazi za ujenzi zinatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Juni, 2025. Kwa sehemu zilizobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kuendelea na ujenzi. Ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved