Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 10 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu 158 2025-02-10

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

Kufanya Mabadiliko kwenye Kikokotoo
cha Watumishi Nchini

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itafanya mabadiliko kwenye Kikokotoo cha Watumishi nchini kwa kuwa kumekuwa na malalamiko mengi?

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 Serikali ilifanya mabadiliko ya Kikokotoo kwa watumishi nchini na mwaka 2024/2025 imefanya maboresho zaidi kwenye kikokotoo hicho baada ya mjadala ndani ya Bunge lako kama ifuatavyo:-

(i) Kuboresha malipo ya mkupuo kutoka 33% hadi 40% kwa waliokuwa wanapata 50% na kutoka 33% hadi 35% kwa waliokuwa wanapata 25% kabla ya kuunganishwa kwa Mifuko mwaka 2018; na

(ii) Mwezi Januari 2025, Serikali imeongeza kima cha chini cha pensheni kutoka shilingi 100,000 hadi shilingi 150,000 kwa mwezi. Vilevile, Serikali imehuisha (indexation) pensheni ya kila mwezi kwa kiwango cha asilimia mbili kwa kuzingatia sheria na Kanuni zilizopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo, naomba kulijulisha Bunge kuwa, Serikali itaendelea kufanya tathmini ya kupima uhimilivu wa Mifuko kila baada ya miaka mitatu kama inavyoelekezwa kisheria ili kuangalia uwezo wa kuboresha mafao bila kuathiri uendelevu wake.