Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 10 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 166 2025-02-10

Name

Neema Kichiki Lugangira

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Kufikisha Umeme wa REA Mashuleni

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. NEEMA K. LUGANGIRA aliuliza:-

Je, Serikali haioni haja kupitia upya Mkataba wa REA kuhakikisha umeme unafikishwa mashuleni ili shule ziunganishwe na huduma za TEHAMA?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatoa kipaumbele katika kufikisha umeme kwenye taasisi zinazotoa huduma kwa jamii zikiwemo Taasisi za Elimu. Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya umeme wa uhakika katika maeneo hayo. Hadi kufikia mwezi Januari, 2025 taasisi za elimu zilizopatiwa umeme kupitia REA ni 18,597. Aidha, Serikali kupitia REA itaendelea kupeleka umeme kwenye vituo vya huduma nchini kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.