Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 3 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 34 | 2025-04-10 |
Name
Felista Deogratius Njau
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Msinga hadi Masoka ili kupunguza adha kwa wananchi wa Moshi Vijijini?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Msinga hadi Masoka imekuwa ikitengewa fedha kwa kufanyiwa matengenezo ya kawaida mara kwa mara kulingana na upatikanaji wa fedha. Kwa mwaka wa fedha 2024/2025, barabara hii imefanyiwa matengenezo ya kawaida kwa kuchonga urefu wa kilometa 0.96 na kuchimba mifereji ya tupa maji (mitre drain) mita 100. Aidha, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imeweka katika mipango yake ya bajeti shilingi milioni 13 kwa ajili ya matengenezo ya kawaida ili kuhakikisha inapitika wakati wote wa mwaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara katika Jimbo la Moshi Vijijini kwa kujenga, kukarabati na kufanya matengenezo kulingana na upatikanaji wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved