Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 3 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 36 2025-04-10

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga minara ya mawasiliano Vijiji vya Lukani na Ng’uluhe - Kilolo ili kuboresha mawasiliano?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia UCSAF ilifanya tathmini ya hali ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali Wilayani Kilolo mwaka 2021/2022 kwa lengo la kubaini maeneo yenye changamoto ya mawasiliano ya simu. Katika tathmini hii ilibaini uwepo wa changamoto katika Kata za Ibumu, Irole, Uhambingeto, Kimala, Mahenge na Masisiwe. Wizara ilijumuisha Kata hizo kwenye Mradi wa Ujenzi wa Minara 758 katika kata 753 unaotekelezwa kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa mradi katika Kata mbili za Irole na Masisiwe umekamilika na utekelezaji katika kata nyingine nne unaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Wizara kupitia UCSAF ipo katika maandalizi ya kutekeleza mradi wa awamu ya kumi, hivyo Kata ya Ng’uluhe hususan maeneo ya Vijiji vya Lukani na Ng’uluhe alivyovitaja Mheshimiwa Mbunge vitaingizwa katika zabuni hii ya awamu ya kumi ambapo utekelezaji wake unatarajiwa kufanyika katika mwaka wa fedha 2025/2026. Ahsante.