Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 86 2025-04-16

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Primary Question

MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza: -

Je, lini Barabara ya Lake Oil - Ijuganyodo hadi Kyamunene itajengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2024/2025 Barabara ya Lake Oil – Ijuganyodo hadi Kyamunene imetengewa shilingi milioni 40 kwa ajili matengenezo ya changarawe urefu wa kilometa 2.078 na ujenzi wa mifereji mita 800. Aidha, mkandarasi wa kazi hiyo ameshapatikana na anatarajiwa kuanza hivi karibuni. Katika mwaka 2025/2026 barabara hiyo pia imewekwa kwenye mpango wa bajeti kwa kutengewa shilingi milioni 33 kwa ajili ya matengenezo ya kiwango cha changarawe urefu wa kilometa mbili ili kukamilisha urefu wa kilometa 4.078.