Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 21 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 265 | 2025-05-09 |
Name
Maimuna Ahmad Pathan
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha barabara za mitaani zinafanyiwa ukarabati na maboresho ili kuepusha usumbufu wakati wa mvua?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka 2021/2022, Serikali iliongeza bajeti ya TARURA kutoka shilingi bilioni 275 hadi shilingi bilioni 870.3 ongezeko la shilingi bilioni 595.3, sawa na 216%, lengo likiwa ni kuijengea uwezo TARURA kuzihudumia barabara zake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali hutenga fedha ya dharura shilingi bilioni 21 katika bajeti kila mwaka ili kukabiliana na athari zinazosababishwa na mvua. Katika mwaka 2023/2024 Serikali ilitoa shilingi bilioni 84.36 kutokana na mvua za El Nino zilizoleta madhara makubwa katika barabara hapa nchini na katika mwaka wa fedha 2024/2025 imetoa shilingi bilioni 11.6.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuujengea uwezo wa kibajeti wa TARURA kulingana na upatikanaji wa fedha ili uweze kuzikarabati barabara za mitaa na kuwa tayari hasa nyakati mvua za masika na vuli zinaponyesha, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved