Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 10 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 120 | 2025-04-23 |
Name
Anton Albert Mwantona
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Rungwe
Primary Question
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza kusajili wanafunzi katika shule ya Msingi ya Ushirika Kata ya Mpuguso iliyojengwa kwa nguvu za w ananchi?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Shule ya Msingi ya Ushirika ilisajiliwa rasmi tarehe 9 Januari, 2024 na kupewa namba ya usajili EM.20614, kwa barua yenye kumbukumbu Na. EA.295/315/20A/32 ya tarehe 9 Januari, 2024.
Mheshimiwa Spika, shule hiyo ilianza kupokea wanafunzi tarehe 5 Februari, 2024. Kwa sasa shule ina jumla ya wanafunzi 138, wakiwemo wavulana 74 wasichana 64 ambao wako darasa la awali hadi darasa la tatu.
Mheshimiwa Spika, Serikali inawapongeza wananchi wa Kata ya Mpuguso kwa michango na jitihada zao zilizowezesha upatikanaji wa elimu karibu na maeneo yao.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved